Bekele ajiandaa kwa mbio za Paris marathon | Michezo | DW | 04.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bekele ajiandaa kwa mbio za Paris marathon

Katika riadha mwanariadha shujaa wa Ethiopia Kenenisa Bekele anasema yuko katika hali nzuri na anatarajia kushinda mbio zake za kwanza kabisa za marathon kwenye barabara za Paris Jumapili

Mwanariadha huyo aliyeweka rekodi mbili za ulimwengu katika mbio za mita 5,000 na 10,000 ataangaziwa macho katika mbio hizo za Paris Marathon, kuona kama atafaulu kufanya vyema katika marathon. Anasema ana nafasi nzuri kwa sababu amefayna mazoezi ya kutosha na atakimbia ili kupata ushindi.

Baada ya kuwa na taaluma nzuri katika mbio za masafa mafupi, mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 31 anataraji kufuata nyayo za Mfalme wa Ethiopia Haile Gebreselassie, ambaye alifaulu kubadilisha taaluma yake kutoka mbio za uwanjani hadi zile za marathon.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman