BEIT HANOUN: Mashambulio ya Israel yameua wanamgambo wa Hamas | Habari za Ulimwengu | DW | 05.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIT HANOUN: Mashambulio ya Israel yameua wanamgambo wa Hamas

Vikosi vya Kiisraeli vimewauwa wanamgambo 7 wa Hamas na raia 2 katika mashambulio yaliofanywa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.Sasa idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulio ya Israel ya siku nne kwenye mji wa Beit Hanoun imefikia 44.Mwanajeshi mmoja wa Kiisraeli pia ameuawa.Jeshi la Israel linasema,mji wa Beit Hanoun umelengwa kwa sababu mashambulio mengi ya makombora dhidi ya Israel yanafanywa kutoka mji huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com