BEIRUT:Upinzani wataka uchaguzi wa mapema Lebanon | Habari za Ulimwengu | DW | 19.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT:Upinzani wataka uchaguzi wa mapema Lebanon

Upinzani nchini Lebanon ukiongozwa na kundi linaloungwa mkono na Syria la Hezbollah limetaka kufanyike uchaguzi wa mapema ili kuutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Wito huo wa Hezbollah umetolewa baada ya serikali ya Lebanon ya waziri mkuu Fuad Siniora inayoungwa mkono na nchi za magharibi kukataa kukubali kuunda serikali mpya ya umoja wa kitaifa.

Wafuasi wa ngome ya upinzani wamekuwa wakifanya maandamano ya umma katika mji wa Beirut tangu desemba mosi wakitishia kuipindua serikali wasiyoitambua baada ya kujiuzulu mawaziri sita wanaoegemea upande wa Syria.

Mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu Amr Moussa amekuwa akijaribu kupatanisha katika mzozo huo wa kisiasa kati ya makundi hayo mawili lakini hajafanikiwa kupiga hatua kubwa katika usuluhishi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com