BEIRUT:Maandamano ya Hezbollah yaisha Beirut | Habari za Ulimwengu | DW | 24.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT:Maandamano ya Hezbollah yaisha Beirut

Wafuasi wa upinzani nchini Lebanon wamemaliza mgomo na kufungua barabara kufuatia siku nzima ya maandamano hapo jana.Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Syria liliitisha maandamano hayo ili kuonya serikali ya Lebanon inayoongoza na Waziri Mkuu Fouad Siniora anayeungwa mkono na Marekani.Vyama vya upinzani vinapinga uongozi wa Bwana Siniora na kumtaka ajiuzulu vilevile kudai uundwaji wa serkali ya kitaifa.Yapata watu watatu wameuawa na wengine kujeruhiwa wakati ghasia zilipozuka barabarani kati ya wafuasi wa serikali na wapinzani wake mjini Beirut.Ghasia hizo ndizo mbaya zaidi kutokea tangu kundi la Hezbollah kujaribu kumshinikiza Waziri Mkuu Fouad Siniora kujiuzulu.Bwana Siniora kwa upande wake anashikilia kuwa hatatishika.

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anatoa wito kwa vyama vyote nchini Lebanon kurejea katika mazungumzo ili kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa unaokumba taifa hilo. Kiongozi huyo anatashwishi na hali hiyo kwani hayo yanatokea wakati mkutano wa wafadhili unafanyika mjini Paris.Lebanon inataraji kwamba itapata ufadhili ili kuimarisha uchumi wake unaoregarega kufuatia vita kati ya Hezbollah na Israel mwaka jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com