1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Steinmeier atoa wito kuheshimiwa utaifa wa Lebanon.

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn9

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amekuwa mjini Beirut kwa mazungumzo na viongozi wa Lebanon.

Baada ya kukutana na mwanasiasa wa Kishia wa upinzani Nabih Berri, ambaye ni mshirika la kundi la Hizboullah, ametoa wito kwa mataifa mengine kuheshimu utaifa wa Lebanon.

Amesema kuwa kuidhoofisha serikali ya Lebanon hakutakuwa na manufaa kwa yeyote.

Kufuatia mkutano wake na waziri mkuu Fouad Siniora , Steinmeier anatarajiwa kwenda nchini Cypruss, ambako atalitembelea jeshi la majini la Ujerumani ambalo linasaidia ulinzi katika pwani ya Lebanon. Kabla ya kwenda Beirut Steinmeier alitembelea eneo la Gaza , ambako alitoa wito wa kufufuliwa kwa hatua za kuleta amani katika mashariki ya kati.