Beirut. Rais akataa kuidhinisha pendekezo la kuunda mahakama. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Beirut. Rais akataa kuidhinisha pendekezo la kuunda mahakama.

Rais wa Lebanon anayeiunga mkono Syria Emile Lahoud amekataa kuidhinisha mipango ya serikali ya kuundwa kwa mahakama ya kimataifa kuwahukumu watuhumiwa wa mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Rafik Hariri.

Rais huyo amehalalisha uamuzi wake, akisema kuwa baraza la mawaziri ambalo limeondokewa na mawaziri kadha halina uhalali kikatiba kuidhinisha hatua kama hiyo.

Mwezi uliopita , mawaziri sita ambao wanaiunga mkono Syria wamejitoa katika serikali na mawaziri waliobaki wameidhinisha pendekezo hilo la kuwa na mahakama hiyo.

Mahakama hiyo ndio chanzo cha mzozo baina ya serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na upinzani, ambao umekuwa ukifanya maandamano kila siku wakijaribu kumuondoa waziri mkuu ambaye anaipinga Syria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com