BEIRUT: Matumaini ya kuundwa serikali ya umoja ya Wapalestina | Habari za Ulimwengu | DW | 14.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Matumaini ya kuundwa serikali ya umoja ya Wapalestina

Msomi wa Kipalestina Mohamed Shbair anatazamiwa kuchukua nafasi ya waziri mkuu wa hivi sasa wa chama cha Hamas,Ismail Haniyeh.Maafisa wa Kipalestina wamesema Shbair ambae hapo zamani alikiongoza chuo kikuu cha kiislamu cha Gaza amekubali kupokea cheo cha waziri mkuu.Lakini rais Mahmoud Abbas mwenye siasa za wastani kutoka chama cha Fatah kilichotawala hapo zamani, atahitaji kutoa idhini yake.Ni matumaini ya Wapalestina kuwa waziri mkuu mpya na serikali ya umoja wa kitaifa,ni mambo yatakayosaidia kuzifanya nchi za magharibi kuregeza vikwazo vilivyowekwa baada ya Hamas kushika madaraka mwezi wa Machi.Marekani na Umoja wa Ulaya zimekitaka chama cha Hamas kitambue haki ya kuwepo taifa la Israel,kitangaze kuacha matumizi ya nguvu na kiheshimu mikataba ya amani iliyotiwa saini na Israel,ili vikwazo viweze kuondoshwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com