1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Mabasi mawili ya abiria yashambuliwa kwa mabomu

13 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSc

Watu kati ya 3 na 12 wameuwawa na wengine 10 wamejeruhiwa wakati mabasi mawili ya abiria yaliporipuka katika kijiji cha Ain Alak nchini Lebanon.

Mashambulio hayo yamefanika huku taifa likijiandaa hapo kesho kuadhimisha mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri, aliyeuwawa kwenye shambulio la bomu miaka miwili iliyopita.

Kijiji hicho kiko karibu na mji wa Bikfaya alikozaliwa rais wa zamani wa Lebanon, Amin Gemayel, katika maeneo ya milimani karibu na mji mkuu Beirut.

Mripuko wa kwanza umetokea mwendo wa saa tatu na nusu ndani ya basi lililokuwa limeja abiria na dakika saba baadaye bomu lengine likaripuka ndani ya basi lengine la abiria lililokuwa karibu.

Msemaji wa jeshi la Lebanon ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema haijabainika wazi ikiwa mabomu hayo yalikuwa ndani ya mabasi au yalikuwa yametegwa kando ya barabara.