1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Lebanon yalalamika Israel inavunja makubaliano.

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD54

Lebanon imeutaka umoja wa mataifa kuweka mbinyo kwa Israel kuacha kuenda kinyume na makubaliano ya kutoingia katika anga yake na kuondoa majeshi yake yote kutoka Lebanon.

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora amesema kuwa Israel inakiuka azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa 1701, ambalo lilimaliza vita vya siku 33 baina ya kundi la wapiganaji la Hizboullah na Israel mwezi wa August.

Israel inasema kuwa haitaacha kurusha ndege zake katika anga ya Lebanon hadi pale kundi la Hizboullah litakapowaacha huru wanajeshi wawili waliokamatwa Julai 12.

Siku ya Ijumaa , ndege za kivita za Israel ziliruka chini chini katika bonde la Bekaa na maeneo karibu na kusini mwa Lebanon.