1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Jeshi laendelea na operesheni ya kuwangóa wanamgambo

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpD

Jeshi la Lebanon limesema,linaendelea na operesheni za kijeshi katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr al-Bared,kaskazini mwa Lebanon.Lengo la operesheni hiyo ni kuwangóa wapiganaji wa kundi la Fatah al-Islam waliobakia katika kambi hiyo.Hapo awali,waziri wa ulinzi wa Lebanon alisema,wanamgambo hao wa Kiislamu waliojificha kambini wameshindwa,na sasa jeshi linashughulika na operesheni ya kuisafisha kambi hiyo.