1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Jeshi laanza tena kushambulia wanamgambo

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxs

Marekani imepeleka silaha zaidi nchini Lebanon hapo jana ambapo jeshi la nchi hiyo linapambana kuwashinda wanamgambo wa Kiislam wenye silaha nzito waliojichimbia ndani ya kambi ya wakimbizi wa Wapalestina ya Nahr al Bared.

Kundi la wanamgambo la Fatah al Islam ambalo limeapa kupambana hadi kifo limesema katika taarifa kwamba silaha hizo za Marekani zinajumuisha gesi ya kuuwa mishipa ya fahamu na mabomu ya mtawanyo.

Taarifa hiyo iliosomwa na msemaji wa kundi hilo Abu Salim Taha imesema iwapo watatumia silaha zisizo za kawaida watajibu mapigo kwa mashambulizi ya silaha zisizo za kawaida kila mahala.

Habari zinasema wanajeshi wa Lebanon wameanza tena kuwashambulia wanamgambo hao kwenye kambi hiyo ya Wapalestina na kuvunja suluhu iliodumu kwa siku nne.

Mapigano hayo ambayo ni umgwaji damu mkubwa kabisa wa ndani ya nchi tokea vita vya wenyewe wenyewe vya Lebanon vya mwaka 1975 hadi mwaka 1990 yameuwa takriban watu 75.