BEIRUT: Hezbollah kuitisha maandamano dhidi ya serikali | Habari za Ulimwengu | DW | 13.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Hezbollah kuitisha maandamano dhidi ya serikali

Mazungumzo juu ya Korea ya Kaskazini kuacha mpango wake wa nyuklia

Mazungumzo juu ya Korea ya Kaskazini kuacha mpango wake wa nyuklia

Rais wa Lebanon anaeiunga mkono Syria amezidisha mgogoro wa kisiasa wa nchi yake kwa kusema kuwa baraza la mawaziri la waziri mkuu Fouad Siniora si halali tena.Rais Emile Lahoud katika barua aliopeleka kwa waziri mkuu amesema,serikali imepoteza uhalali wake kwa sababu kuambatana na katiba,baraza la mawaziri lazima liwe na idadi sawa sawa ya Wakristo na Waislamu.Mawaziri watano walijiuzulu baada ya kutofanikiwa kuimarisha serikalini,ushawishi wa chama chao kinachoiunga mkono Syria.Waziri mkuu Fouad Siniora amekataa kukubali kujiuzulu kwa mawaziri wa Hezbollah na Amal na amesisitiza kuwa anataka kufanya kazi pamoja na vyama vyote kwa azma ya kuumaliza mgogoro wa nchi hiyo.Kwa upande mwingine Wahezbollah wamesema wataitisha maandamano makubwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com