1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Fouad ameamrisha kuteketeza wapiganaji

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzb

Serikali ya Lebanon imetoa amri kwa vikosi vyake kuliteketeza kundi la “Fatah al-Islam”.Kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri,ulioongozwa na waziri mkuu Fouad Siniora,serikali ilisema,vita vya magaidi lazima vikomeshwe.Kwa siku ya tatu kwa mfululizo,vikosi vya serikali na wanamgambo wa madhehebu ya Kisunni wanapigana vikali kaskazini mwa Lebanon.Tangu mapambano kuzuka katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr-al-Bared,kiasi ya watu 80 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa.Msemaji wa wanamgambo hao ameonya kuwa kutazuka vita vya wenyewe kwa wenyewe,ikiwa serikali haitosita kuishambulia kambi hiyo ya wakimbizi,ambayo ni ngome ya kundi hilo.