1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Uchina yaghadhabishwa na Marekani kuhusu Dalai Lama

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ey

Uchina inatoa matamshi mapya makali kufuatia uamuzi wa Marekani wa kumtuza kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama aidha kufanya naye mkutano mjini Washington katika Ikulu ya Whitehouse hapo jana.China kwa upande wake haijaridhia hatua hiyo na kushikilia kuwa sherehe hiyo isimamishwe.Liu Jianchao ni msemaji wa Wizara ya Mambo ya kigeni ya Uchina.

''Uchina haijafurahia ziara hii kwani inafanyika sawasawa na wakati ambapo kongamano la vyama 17.Vyombo vya habari vingepaswa kutangaza hatua zilizopigwa .Kulingana na Uchina hatua hii ni ukosefu wa uaminifu kwa upande wa Marekani''

Kwa mujibu wa Uchina Dalai Lama ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani ya mwaka 1989 anashikilia kudai uhuru wa kujisimamia katika eneo la Tibet ila chini ya utawala wa Kichina.

Rais George Bush wa Marekani na wabunge wa ngazi za juu nchini humo wanajiandaa kumtuza rasmi kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama jambo linalotishia uhusiano kati ya Uchina na Marekani.Kiongozi huyo wa kidini anatarajiwa kutuzwa medani ya dhahabu ambayo ni tuzo la hadhi ya juu kabisa kupewa raia wa kawaida na bunge la Marekani.Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani aliye madarakani kukutana rasmi na kiongozi huyo wa Kibudda aliye na umri wa miaka 72.Lengo la hatua hiyo ni kumtuza kiongozi wa kidini wa Tibet vilevile kuafiki uhuru wa kidini katika eneo la Tibet.Dana Perino ni msemaji wa Ikulu ya Whitehouse

''Hatutaki kusababisha mvutano wowote na kuifanya Uchina kuhisi kuwa tunaingilia mambo yao ya ndani.Rais Bush anafahamu kwamba jambo hili linazua hisia tofauti na kama kiongozi na rais wa Marekani anayehudhuria vikao vya bunge huenda akashuhudia kitendo hicho cha kumtuza''

Dalai Lama alitorokea nchi ya India baada ya jaribio la mapinduzi dhidi ya uongozi wa Uchina mwaka 1959.Kiongozi huyo wa kidini anaishi mjini Dharamsala kwa sasa ambako ndiko makao makuu ya serikali yake ya uhamishoni.Uchina iinamiliki eneo la Tibet lililo na wafuasi wengi wa Kibudda tanghu ilipotuma majeshi yake huko mwaka 1950.