BEIJING:Korea kaskazini yabakia ngangari juu ya mpango wake wa Kinuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 19.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING:Korea kaskazini yabakia ngangari juu ya mpango wake wa Kinuklia

Mjumbe wa Korea kaskazini kwenye mazungumzo ya pande sita kuhusu mpango wa Nuklia wa nchi hiyo,Kim Kye-Gwan amesema nchi yake inataka vikwazo vyote dhidi yake viondolewe kabla haijaingia kwenye majadiliano ya kuachana na mpango wake wa Kinuklia.

Mjumbe huyo wa Korea Kaskazini ameonya endapo hilo halitafanyika basi nchi yake itapanua uwezo wake wa kinuklia.

Marekani imeitaka Korea kaskazini kukomesha mpango wake wa kinuklia la sivyo ichukuliwe hatua.

Korea Kaskazini ilijiondoa kwenye mazungumzo ya pande sita mwezi Novemba mwaka jana ikipinga vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Marekani na baadae Octoba 9 ikafanya jaribio lake la kwanza la silaha za kinuklia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com