BEIJING:19 wafa katika mlipuko kwenye mgodi wa makaa ya mawe | Habari za Ulimwengu | DW | 29.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING:19 wafa katika mlipuko kwenye mgodi wa makaa ya mawe

Kumetokea mlipuko wa gesi kwenye mgodi mmoja wa makaa ya mawe huko China ambapo wachimbaji 19 wameuawa na wengine 9 hawajulikani walipo.

Shirika la habari la China limearifu kuwa , tukio hilo limetokea katika mgodi wa Linfei katika jimbo la Shanxi, ikiwa ni siku 10 tu baada ya tukio lingine kama hilo, lililopelekea vifo vya wachimbaji 21.

Migodi ya makaa ya mawe nchini China ni migodi hatari duniani, ikiwa na matukio ya kila siku, ya milipuko na mafuriko, pamoja na serikali ya nchi hiyo kuahidi kuboresha hali hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com