1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Watu takriban 22 wauwawa

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZP

Watu takriban 22 wameuwawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa baada ya daraja kuanguka kusini mwa China. Madarzeni wa watu wanasemekana hawajulikani waliko huku kukiwa na hofu ya idadi ya vifo kuongezeka.

Daraja hiyo, ambayo ilikuwa bado haijamalizika kujengwa, iko katika wilaya ya Fenghuang, kivutio muhimu cha watalii kwenye mkoa wa Hunan.

Shirika rasmi la habari la China, Xinhua, limesema haikubainika wazi kilichosababisha ajali hiyo lakini uchunguzi umeanza kutafuta chanzo chake.