BEIJING: Mvua kubwa zasababisha mafuriko kusini mwa China | Habari za Ulimwengu | DW | 23.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING: Mvua kubwa zasababisha mafuriko kusini mwa China

Hadi watu 49 wamefariki katika mafuriko na mmomonyoko wa ardhi uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kusini mwa China.Katika mji wa Chongqing na wilaya za Hubei,Sichuan na Guizhou watu 23 wanakosekana.Kiasi ya watu milioni 10 wameathirika na zaidi ya wakazi 400,000 wamehamishwa sehemu zingine.Watu 128 pia walipoteza maisha yao juma lililopita katika mafuriko yaliyotokea sehemu zingine za eneo la kusini nchini China.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com