1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Motokaa zapigwa marufuku

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYN

Serikali ya mjini Beijing imepiga marufuku motokaa zaidi ya milioni moja katika barabara za mji huo katika jaribio la kuimarisha ubora wa hewa kwa ajili ya michezo ya Olimpik.

Zaidi ya maafisa 6,500 wa polisi wametumwa kushika doria kuhakikisha wenye magari wanatii amri hiyo. Kuanzia leo hadi Jumatatu ijayo, takriban magari milioni 1.3 kati ya magari milioni tatu ya mjini Beijing hayataruhusiwa katika barabara za mjini Beijing.

Mji huo umeathiriwa na uchafuzi wa hewa na moshi ambao ni kikwazo kikubwa kwa wachezaji na wageni watakaokwenda kushiriki kwenye michezo ya Olimpik itakayofanyika mwaka ujao.

Jaribio hilo la siku nne linatangulia juhudi nyingine zitakazofanywa wakati wa mashindano ya Olimpik mwakani.