1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHong Kong

Beijing ina mashaka na mawakili wakigeni Hong Kong

Saumu Mwasimba
29 Novemba 2022

Kiongozi wa Hong Kong John Lee amesema serikali kuu mjini Beijing ina mashaka makubwa kuhusu suala la kuhusika kwa mawakili wa kigeni katika kesi ambazo zinagusa suala la usalama wa taifa.

https://p.dw.com/p/4KDfc
Hongkong | 25. Jahrestag der Rückgabe an China
Picha: Selim Chtayti/REUTERS

Kiongozi huyo John Lee jana aliliomba  bunge la taifa la watu wa China ambalo ndio mamlaka ya mwisho kutowa uamuzi kuhusu ombi la HongKong la kutaka kuzuia mawakili wa kigeni kushughulika katika kesi zinazogusa suala la usalama wa taifa.

Hatua hiyo inakuja baada ya mahakam ya juu katika mji huo wa HongKong kupitisha uamuzi kwamba wakili mmoja raia wa Uingereza anaweza kumuwakilisha bilionea Jimmy Lai aliyeko jela na ambaye ni mpiganiaji demokrasia.

Kesi ya Lai itasikilizwa alhamisi. Kiongozi wa Hong Kong John Lee amewaambia waandishi habari leo kwamba anatarajia kamati kuu ya bunge la umma wa China NPC,kufanya maamuzi kuhusu suala hilo.