BEIJING: El-Baradei amekatisha ziara ya Korea ya Kaskazini | Habari za Ulimwengu | DW | 14.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING: El-Baradei amekatisha ziara ya Korea ya Kaskazini

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa,bwana Mohammed el-Baradei amekatisha majadiliano yake nchini Korea ya Kaskazini na amekwenda Beijing nchini China.Mazungumzo hayo yamehusika na mradi wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini.Inasemekana kuwa el-Baradei amekatisha ziara yake kwa sababu hakuweza kukutana na naibu waziri wa nje wa Korea ya Kaskazini,Kim Kye Gwan ambae ni mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya mradi wa nyuklia wa nchi hiyo.Serikali mjini Pyongyang imesem,waziri Kim hakuweza kuonana na el-Baradei kwa sababu ana shughuli nyingi sana.Badala yake,El-Baradei alionana na afisa mwengine anaefanya kazi pamoja na Kim.Baada ya kupatikana makubaliano ya kusitishwa mradi wa nyuklia wa Korea ya kaskazini,el-Baradei alitaka kulijadili suala la kuwaruhusu wakaguzi wa nyuklia kurejea nchini humo hivi karibuni.Katika mazungumzo yaliyofanywa kati ya nchi sita ikiwa ni pamoja na Korea ya Kaskazini,serikali ya Pyongyang ilikubali kuwa hadi katikati mwezi Aprili,itakifunga kabisa kinu chake cha nyuklia cha Yongbyon.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com