BEIJING: Condoleezza Rice amewasili nchini China | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING: Condoleezza Rice amewasili nchini China

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice akiendelea na ziara yake barani Asia,leo hii amewasili China.Rice anataka kuisadikisha Beijing iliyo na shaka,iishinikize Korea ya Kaskazini kuhusu mradi wake wa kinuklia. Rice amewasili China siku moja baada ya tume ya maafisa wa ngazi ya juu kupelekwa Korea ya Kaskazini na ujumbe wa serikali ya Beijing.Kwa mujibu wa maafisa wa Kimarekani,tume hiyo imekwenda na ujumbe mkali,baada ya Korea ya Kaskazini kufanya jaribio lake la kinuklia wiki iliyopita.

Waziri Rice kabla ya kuelekea China kwa mara nyingine tena alitoa mwito wa kutekelezwa kikamilifu vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea ya Kaskazini.Wakati huo huo akasisitiza dhamira yake ya kutafuta suluhisho la kidplomosia kuhusu mgogoro wa kinuklia wa Korea ya Kaskazini.Baraza la Usalama lilipiga kura kuiwekea vikwazo Korea ya Kaskazini baada ya nchi hiyo kutangaza kuwa ilifanya jaribio la kinuklia tarehe 9 mwezi huu wa Oktoba.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com