1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. China yapata waziri mkuu mpya.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6R

China imemtangaza balozi wa zamani nchini Marekani kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo, akichukua nafasi ya mwanadiploamsia veterani Li Zhaoxiang.

Inafikiriwa kuwa yang Jiechi , anaweza kusaidia kuweka sawa hali ya mvutano na Marekani kuhusiana na masuala ya biashara, matumizi ya kijeshi na malengo ya muda mrefu ya China.

Yang , mwenye umri wa miaka 56 , ametumikia ubalozi wa China mjini Washington katika miaka ya 1980 na 1990, na kurejea tena kama balozi katika mwaka 2001 na 2005.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kwa kuondolewa kwa Li, katika akiwa na umri wa miaka 66 alikuwa kwa kiasi kikubwa akitarajiwa kujiuzulu baadaye mwaka huu ama mapema mwakani. China imekuwa ikijenga mahusiano mazuri na majirani zake, ikiwa ni pamoja na Japan na Russia, na imekuwa ikichukua nafasi muhimu katika majadiliano yenye lengo la kumaliza mpango wa kinuklia wa Korea ya kaskazini.