1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING : China na Afrika zasaini mikataba ya biashara ya bilioni 1.9

5 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvr

China na Afrika zimesaini mikataba 16 ya biashara yenye thamani ya dola bilioni 1.9 katika siku ya mwisho ya Mkutano wa Viongozi wa Ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Beijing.

Mapema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amelikaribisha tangazo la China kuongeza maradufu msaada wake kwa Afrika ifikapo mwaka 2009.Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amesema Waafrika wakionyesha kujizatiti kwao upya wanaweza kufaidika kutokana na uzoefu wa China katika uchumi endelevu na kupunguza umaskini.

Mikataba hiyo 16 ya biashara iliotangazwa leo hii na mataifa 10 ya Afrika inahusu ushirikiano katika mali asili, miundo mbinu,masuala ya kifedha, teknolojia,vitambaa na mawasiliano.

Wafanya biashara 1,500 wa China na Afrika wamehudhuria mkutano huo uliokwenda sambamba na mkutano wa viongozi wa taifa wa siku mbili.