Beijing 2008 | Michezo | DW | 15.08.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Beijing 2008

Waafrika wasubiri medali zaidi kutoka Beijing

Michael Phelps ,mshindi wa medali sita za dhahabu

Michael Phelps ,mshindi wa medali sita za dhahabu


Mmarekani Michael Phelps mshindi wa medali sita za dhahabu za Olympik akanusha madai ya kutumia madawa ya kuimarisha misuli,na wanariadha wa Afrika wajiandaa kwa duru za mwanzo mwanzo za mbio za mita,800,mita 1500 na mita 300 kuruka viunzi.Tutazungumza pamoja na Lucy Kabuu Wangui,mshindi wa mbio za mita 10.000 katika michezo ya jumuia ya madola mwaka 2006 mjini Melbourne nchini Australia.Naam ,baada ya medali tatu za fedha za Zimbabwe,mbili za Algeri-fedha na shaba,moja ya Shaba ya Togo na moja ya shaba ya Misri,macho ya mashabiki wa riadha barani Afrika yanakodolewa hii leo mjini Beijing zinakofanyika duru za mwanzo mwanzo za mbio za mita 800 upande wa wanawake,mbio za mita 1500 upande wa wanaume na mita 3000 kuruka viunzi,upande wa wanaume-Fainali za mashindano hayo zitafanyika jumapili ijayo.Lakini homa ya mashabiki imezidi kupanda wakisubiri fainali za mbio za mita elfu leo usiku.Ripota wetu Alex Mwakideu amezungumza na mshindi wa michezo ya Jumuia ya madola mwaka 2006 mjini Melbourne nchini Australia,Lucy Kabuu Wangui kutaka kujua jinsi alivyojitayarisha kwa fainali hiyo.Mrembo huyo wa Kenya anasema amejiandaa ipasavyo tangu nyumbani ingawa analalamika sawa na wanariadha wengine kutokana na hali ya joto iliyoko mjini Beijing.


Lucy Kabuu Wangui atapimana nguvu miongoni mwa wengineo,na bingwa wa dunia wa mita elfu kumi,Tirunesh Dibaba wa kutoka Ethiopia.


Kwa upande mwengine muogeleaji wa Marekani Michael Phelps,aliyejinyakulia medali yake ya sita ya dhahabu hii leo mjini Beijing amekanusha rirpoti za kutumia madawa ya kuimarisha misuli."Watu nawaseme wanachotaja kusema.Nnajua mie nimsafi,"amesema Michael Phelps anaetegemea kunyakua medali mbili zaidi za dhahabu ikiwa ni pamoja na mashindano ya kuogelea mita mia moja kupokezana mara nne,fainali zitakaposhindaniwa jumapili ijayo.


 • Tarehe 15.08.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Exqo
 • Tarehe 15.08.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Exqo