Bayern yapeta; Dortmund hoi | Michezo | DW | 12.11.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern yapeta; Dortmund hoi

Bayern Munich yajiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi ya Ujerumani Bundesliga, Borussia Dortmund yateleza tena, na Bayer Leverkusen yaibuka kidedea.

GttyImages 185347113 MUNICH, GERMANY - OCTOBER 19: (L-R) Bastian Schweinsteiger, Thomas Mueller and Mario Mandzukic of Muenchen celebrate their team's second goal during the Bundesliga match between FC Bayern Muenchen and 1. FSV Mainz 05 at Allianz Arena on October 19, 2013 in Munich, Germany. (Photo by Lennart Preiss/Bongarts/Getty Images)

Wachezaji wa Bayern Munich wakipongezana baada ya ushindi

Katika ligi ya Ujerumani Bundesliga , jana Jumapili(10.11.2013) kulikuwa na michezo miwili ya kukamilisha duru ya 12 ya mchezo wa Bundesliga, ambapo Stuttgart iliikaribisha Freiburg. VFB Stuttgatr iliikabidhi Freiburg kipigo cha mabao 3-1 na kupanda hadi katikati ya msimamo wa ligi hiyo. Mainz 05 ikapata ushindi wa jasho wa bao 1-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt ikiwa ni ushindi wa dakika za mwisho.

WOLFSBURG, GERMANY - NOVEMBER 09: Ivica Olic of Wolfsburg and neven Subotic (#4) of Dortmund battle for the ball during the Bundesliga match between VfL Wolfsburg and Borussia Dortmund at Volkswagen Arena on November 9, 2013 in Wolfsburg, Germany. (Photo by Martin Rose/Bongarts/Getty Images)

Siku Borussia Dortmund iliposalim amri mbele ya Wolfsburg

Choupo-Moting alipachika bao hilo la ushindi zikiwa zimesalia sekunde 120 mchezo kumalizika. Hata hivyo mlinda mlango chipukizi wa Mainz 05 Loris Karius ambaye alikuwa langoni badala ya kipa namba moja Heinz Müller ambaye ni majeruhi na kipa namba mbili Christian Wetklo ambaye ana kadi nyekundu alifanya kazi nzuri kulinda ushindi huo.

"Sikuwa na wasi wasi. Nilikuwa nafahamu kwa siku kadha kuwa nitacheza na nimejaribu, kuweka yote hayo pamoja. Nilikuwa na hisia kuwa itakuwa siku nzuri.Kwa hiyo nilifanya kila linalowezekana."

Siku ya Jumamosi FC Bayern iliiadhibu FC Augsburg kwa mabao 3-0 na kuendelea kujikita kileleni mwa Bundesliga baada ya makamu bingwa wa ligi hiyo Borussia Dortmund kuteleza , baada ya kuzabwa mabao 2-1 na Wolfburg. FC Bayern imeendelea kuvunja rekodi moja baada ya nyingine msimu huu, ambapo wiki hii iliivuka rekodi ya kale iliyokuwa imewekwa na Hamburg SV na kupata ushindi katika michezo 37 ya ligi bila kushindwa.

Leverkusen imeendelea kubakia katika nafasi ya tatu baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 5-3 dhidi ya Hamburg SV. Mshambulia Son alipachika mabao 3 dhidi ya timu yake hiyo ya zamani. Schalke 04 nayo ilijipatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Werder Bremen.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / ape /afpe

Mhariri: Mohammed Khelef