1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yakasirishwa na tangazo la Flick

Bruce Amani
19 Aprili 2021

Bodi ya usimamizi wa Bayern wapinga uamuzi wa kocha Hansi Flick kutangaza hadharani nia yake ya kuondoka mwishoni mwa msimu. Bayern imesema watafanya mazungumzo na Flick kuhusu nia hiyo

https://p.dw.com/p/3sEIm
Trainer Hansi Flick FC Bayern München
Picha: Stefan Matzke/sampics/picture alliance

Bayern Munich huenda wanaelekea kubeba ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya tisa mfululizio, lakini huenda msimu ujao wasiwe na mtu atakayewaongoza kufanya hivyo.

Bodi ya usimamizi wa klabu hiyo imepinga uamuzi wa kocha Hansi Flick kutangaza hadharani nia yake ya kuondoka mwishoni mwa msimu. Flick alitangaza Jumamosi baada ya ushindi wa 3 – 2 dhidi ya Wolfsburg kuwa hataki kuumaliza mkataba wake utakaokamilika mwaka wa 2023.

Bayern imesema jana ni kweli Flick amewaifahamisha bodi hiyo kuhusu nia yake ya kuondoka, lakini inapinga uamuzi huo wa upande mmoja na kwa hiyo wataendelea kufanya mazungumzo.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 anahusishwa na kazi ya timu ya taifa, ambayo itakuwa wazi wakati bosi wake wa zamani Joachim Loew atajiuzulu baada ya mashindano ya Ulaya mwaka huu. Flick alikuwa naibu wa Loew kuanzia 2006 hadi 2014.

Inadokezwa kuwa kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann huenda atakuwa mrithi wa Flick isipokuwa mwenyewe amesema hajawa na mawasiliano na Bayern.

Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters