Bayern watekwa sare, Dortmund wateleza | Michezo | DW | 07.10.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern watekwa sare, Dortmund wateleza

Bayern Munich inaongoza Bundesliga baada ya kutoka sare ya 1-1 na Bayer Leverkusen. Borussia Dortmund nao walipigwa na butwaa baada ya kichapo cha kwanza cha mabao 2-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach.

Bayern, ambao walishindwa na Leverkusen katika ligi msimu uliopita, sasa wamecheza mechi 33 bila kushindwa. Wana pointi 20 baada ya mechi nane, ikiwa ni moja mbele ya Dortmund na nambari mbili Leverkusen.

Bayern Munich waliwachana na mambo ya mpira na kuangazia pombe, wakati wachezaji na wafanyakazi wengine wa klabu hiyo walipojumuika na wengine katika sherehe za kila mwaka za utamaduni wa jimbo la Bavaria, zinazofahamika kama Oktoberfest. Kocha Pep Guardiola alivalia mavazi ya kitamaduni akiandamana na mkewe, wakati pia wachezaji wakisherehekea na familia zao.

Schalke 04 wako katika nafasi ya nane baada ya ushindi wa nyumbani dhidi ya Augsburg

Schalke 04 wako katika nafasi ya nane baada ya ushindi wa nyumbani dhidi ya Augsburg

Nayo Eintracht Braunschweig ilishangaza kwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Wolfsburg, ukiwa ndio ushindi wao wa kwanza tangu walipopandishwa daraja msimu huu.

Schalke walitoka nyuma na kuwazaba Augsburg mabao manne kwa moja katika mechi iliyobadilishwa mkondo kufuatia kadi nyekundu aliyolishwa mchezaji wa Augsburg Ragnar KLAVAN na kisha Kevin Prince Boateng akafunga penalty. Mainz walitoka nyuma na kulazimisha sare ya mabao mawili kwa mawili na Hoffenheim, wakati nao mpambano kati ya Stuttgart na Werder Bremen ukiishia sare ya kufungana bao moja kwa moja.

Katika mechi zilizochezwa jana, Hamburg iliicharaza Nuremberg mabao matano bila jawabu, ikiwa ni ushindi wa kwanza wa kocha Bert van Marwijk kama kocha wa Hamburg tangu alipochukua usukani kutoka kwa kocha aliyetimuliwa Thorsten Fink. Kocha wa Nuremberg Michael Wiesinger alikuwa na haya ya kusema baada ya kichapo hicho. "Leo kulikuwa na adui aliyetushambulia bila huruma uwanjani. Atika michezo yetu iliyopita huenda mambo yangekuwa angalau tofauti. timu zingine zimetupa nafasi ya kupumua. Ijapokua haikuwa mbaya saana..Inashangaza katika kandanda hata ukicheza vizuri kama leo. Tulishiriki vizuri katika kipindi cha kwanza. Tulikuwa na fursa nyingi hasa pembeni, lakini hatukutumia vyema. Lakini unapopoteza kama huu kwa kufungwa mabao matano kwa sifuri..ni wazimu"

Freiburg wanashikilia mkia kwa pamoja na Eintracht Braunschweig baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja na Eintracht Frankfurt katika mechi nyingine iliyochezwa jana. Nicolas Höfler ni mfungaji wa goli la Freiburg. "Ulikuwa mchezo mkali sana tangu wmanzo. Tulitaka sana kushinda leo, kwa sababu ingekuwa muhimu sana kwetu na kisha tukafungwa bao la kiupuzi kwa kufanya makosa. Kwa bahati nzuri tukapa bao na kurudi nyumbani na pointi moja".

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman