Bayern Munich yanyatia tena taji la Bundesliga | Michezo | DW | 20.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bayern Munich yanyatia tena taji la Bundesliga

Je, leo Munich itatamba mbele ya Karlsruhe ?

default

Lukas Podolski atamba tena.

Bundesliga-Ligi ya Ujerumani iko uwanjani wakati huu huku viongozi wa Ligi-Hertha Berlin wakiania pointi 3 nyengine huko Stuttgart.Oliver Kahn -kipa wa zamani wa taifa azungumza na na uongozi wa Schalke ili kuwa meneja wake-wiki baada ya schalke kumtimua meneja wake wa zamani Mueller.Katika Premier League-Manchester United wana miadi leo na Fulham wakati mahasimu wao waliowakomea mabao 4:1 mwishoni mwa wiki iliopita-FC Liverpool wamevinjari kutamba tena kesho mbele ya Aston villa.

Lukas Podolski, arejea katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ujerumani kitakacho pambana na Liechtenstein na Wales kuania tiketi za kombe lijalo la dunia.Na wanaoandaa Kombe hilo la mwaka 2010 nchini Afrika Kusini,wamepanga mpango mkubwa wa kupiga upatu uuzaji wa tiketi kwanza lakini kwa kombe la Confederations Cup juni hii-likifungua pazia la kombe la mwakani la dunia.

Timu ya Taifa ya Ujerumani itakuwa uwanjani wiki ijayo kuania tiketi yake ya kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini:Kocha wa Ujerumani ,Joachim Loew,amemuita tena chipukizi wa Bayern Munich Lukas Podolski kujiunga na timu ya Taifa :

Lukas Podolski,stadi wa mabingwa Bayern Munich,atakaerejea FC Cologne, mwishoni mwa msimu huu, ameanza kutamba tena baada ya Munich kumchezesha tena hivi karibuni.Hii imefuatia kuumia kwa washambulizi 2 wa Bayern Munich:Mtaliana Luca Toni na mshambulizi wa Taifa wa Ujerumani, Miroslav Klose.Kwa kunawiri tena katika klabu yake ya B.Munich tangu katika champions League hata katika Bundesliga, kocha wa Taifa Joachim Loew,(Lov) amemteua tena Podolski katika kikosi cha Taifa:

Podolski ni mmoja katika kikosi cha wachezaji 23 kitakacho pambana na Liechtenstein na Wales. Kocha Loew alinukuliwa kusema,"Inafurahisha kumuona tena Lukas Podolski akichangia mchezo mzuri katikla Bayern Munich."

Ujerumani itacheza na Liechtenstein mjini Leipzig hapo Machi 28 na halafu itafunga safari hadi Cardiff,siku 4 baadae kwa miadi na Wales ili kukata tiketi ya kombe lijalo la dunia huko Afrika Kusini.

Ujerumani inaongoza kundi la 4 la Ulaya ikiwa na pointi 10 kutoka mechi 4 ikifuatwa na Urusi na Wales ambazo kila moja ina pointi 6.Mshindi wa kundi hili anakata m,oja kwa moja tiketi ya Kombe la dunia.Ujerumani ikiongozwa na kocha Loew inahitaji kucheza bora zaidi baada ya kulazwa kwa mabao 2-1 na Norway mwezi uliopita wakati wa dimba la kirafiki.Novemba mwaka jana ilichapwa pia mabao 2-1 na Uingereza mjini Berlin.

Kombe la mashirikisho-Confederations Cup- litakalofungua pazia la Kombe la dunia Juni mwakani huko Afrika Kusini,linakaribia: Wanaoandaa Kombe hilo na lkle la Dunia wamepanga wiki hii kuhimiza uuzaji wa tiketi kwa Confederations Cup na kuwatia mashabiki wa dimba jazba zaidi ya Kombe la dunia.

Kamati ya Maandalio ya Kombe la Dunia ya Afrika Kusini kati ya wiki hii, ilishauri mipango ya kuuza tiketi za makundi kwa makampuni na klabu za mashabiki ili kuongeza uuzaji usioridhisha hadi sasa wa tiketi za Confederations Cup.

Kombe hili litaaniwa kuanzia Juni 14 hadi 28 mwaka huu. Mwenyekiti wa Kamati ya maandalio Danny Joordaan,amesema kwamba mipango hiyo imesha idhinishwa na FIFA kufuatia mikutano iliofanyika Zurich jumaane iliopita.FIFA imepokea maombi ya jumla ya tikleti laki 2 tu kati ya tiketi zote laki 6 na 40.000.

Hii licha ya kwamba Kombe la mashirikisho litaingiza mabingwa wa dunia-Itali,mabingwa wa Ulaya 2008 Spian na mabingwa wa Amerika Kusini Brazil.Jordaan alisema lakini, hesabu mpya ya tiketi zilizouzwa kwa Kombe la dunia hapo mwakani ni kubwa zaidi.Kuhusu Kombe la dunia alisema kuna tiketi laki 7 zinazotembezwa kuuzwa wakati huu kwa awamu hii ya kwanza.Maombi ya kununua tiketi yalianza mwezi uliopita na yatapokewa hadi mwishoni mwa mwezi huu.Baadae kura itapigwa kati ya mwezi ujao kuamia jinsi ya kugawa tiketi.

Mapema mwezi huu,serikali ya Afrika Kusini ililalamika kuwa hazifanywi juhudi za kutosha kuhakikisha tiketi zaidi zinauzwa nyumbani.Kombe la Dunia litachezwa katika viwanja 10 mbali mbali nchini Afrika Kusini kuanzia juni 11 hadi finali Julai 11 2010.Litakuwa Kombe la kwanza kabisa kuchezwa barani Afrika tangu Montevideo,Uruguay,1930 lilipoaniwa kwa mara ya kwanza.

Muandishi:Ramadhan Ali

Mhariri:O.Miraji

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com