Bayern Munich kuwavaa Lazio | Michezo | DW | 22.02.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern Munich kuwavaa Lazio

Mechi za Ligi ya Vilabu Bingwa barani Ulaya zitakuwa zinarindima kwa mara nyengine tena Jumanne ambapo mabingwa Bayern Munich watacheza na Lazio ya Italia katika harakati za kupigania kutetea ubingwa wao hapo kesho.

Jumatano Real Madrid ambayo inashikilia rekodi ya kulishinda taji hilo watakuwa wanasafiri kuelekea Italia kucheza na Atalanta na kutokana na masharti ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, Atletico Madrid watacheza mechi yao dhidi ya Chelsea huko Bucharest huku Manchester City wakipambana na Borussia Mönchengladbach huko Budapest.

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com