1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern mabingwa wa Ujerumani kwa mara 10 mfululizo

25 Aprili 2022

Bayern Munich ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga kwa mara ya kumi mfululizo. Hii ni baada ya kuwalaza mahasimu wao wa muda mrefu Borussia Dortmund mabao 3-1 katika uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena.

https://p.dw.com/p/4APql
Fußball Bundesliga | Bayern München v Borussia Dortmund | Bierdusche Nagelsmann
Picha: KERSTIN JOENSSON/AFP/Getty Images

Mabao ya Bayern yalifungwa na Serge Gnabry, Robert lewandowski na Jamal Musiala huku BVB wakipewa la kufutia machozi na Emre Can.

Hii ilikuwa mara ya saba mfululizo kwa Dortmund kufungwa katika uwanja wa nyumbani wa Bayern katika ligi.

Fußball Bundesliga | Bayern München v Borussia Dortmund
Julian Brandt wa Dortmund akipambana na Leon Goretzka wa BayernPicha: Matthias Schrader/AP/picture alliance

Ikumbukwe kwamba Bayern Munich wamenyakua ubingwa huu zikiwa zimesalia mechi tatu msimu wa Bundesliga kufikia mwisho.

Union Berlin waelekea kuparamia nafasi za Champions League

Kwengineko mwanzoni mwa msimu ni wachache ambao wangeamini iwapo Union Berlin watakuwa wanawania mojawapo ya nafasi za kushiriki mashindano ya Ulaya msimu ujao.

Lakini kwa sasa wameshinda mechi nne mfululizo na wamekwea hadi katika nafasi ya sita kwenye jedwali la Bundesliga baada ya ushindi wao mkubwa walipokuwa wakicheza na RB Leipzig ugenini huko mjini Leipzig.

Fußball Bundesliga RB Leipzig v 1. FC Union Berlin
Kevin Behrens akisherehekea kufunga goli la ushindi dhidi ya LeipzigPicha: RONNY HARTMANN/AFP/Getty Images

Huku zikiwa zimesalia mechi tatu msimu kufikia mwisho, Union wako pointi nne tu nyuma ya eneo la kuweza kushiriki Champions League msimu ujao, kwa hali ilivyo sasa watashiriki Conference League.

Bayern mabingwa wa Ujerumani kwa mara 10 mfululizo