1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kucheza licha ya Gnabry kuambukizwa corona

Deo Kaji Makomba
21 Oktoba 2020

Mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa kati ya Bayern Munich dhidi ya Atletico Madrid Jumatano tarehe (21.10.2020) utafanyika kama ilivyopangwa licha ya mchezaji Serge Gnabry kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona

https://p.dw.com/p/3kEhL
DFB Pokal Finale - Bayer Leverkusen vs. Bayern Munich | Tor 0 : 2
Mshambuliaji Serge Gnabry wa timu ya Bayern Munich.Picha: Reuters/J. MacDougal

"Pamoja na upimaji wa kawaida, kila siku, inawezekana kuondoa kanuni uwezekano wa mchezaji aliyeambukizwa kushiriki kwenye mchezo ", yeye kama yeye." alisema Chanasit.

Alipoulizwa ikiwa tayari wachezaji wengine wa Bayern wanaweza kuwa wameambukizwa Schmidt-Chanasit alisema: "Hapana, hiyo pia ingegunduliwa mapema sana. "

Daktari wa virusi alielezea kuwa mmoja wa wachezaji bado anaweza kuwa ndani kipindi cha kufikia dalili za virusi kuonekana, lakini maambukizo zaidi yanaweza kutolewa na kipimo hasi cha PCR.

Mshambuliaji wa Bayern Gnabry alikutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo Jumanne iliyopita na bila shaka atakosa mechi ya Jumatano tarehe (21.10.2029) ya Ligi ya Mabingwa dhidi Atletico Madrid na mechi ya Jumamosi ya Bundesliga na Eintracht Frankfurt, lakini labda pia michezo zaidi wiki ijayo.

Gnabry alifanya mazoezi na timu Jumanne asubuhi na kama matokeo yote wachezaji watalazimika kupitia kipimo kingine cha virusi vya corona kabla ya mechi ya Atletico. Kulingana na itifaki ya UEFA, Bayern lazima iwasilishe vipimo kwa wachezaji wote saa sita kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Chanzo/DPAE