Bayern, Atletico zajikatia tikiti ya nusu fainali | Michezo | DW | 14.04.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bayern, Atletico zajikatia tikiti ya nusu fainali

Bayern Munich imetinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya mabao mawili kwa mawili na Benfica Lisbon jana usiku. Munich walifuzu kwa jumla ya mabao matatu kwa mawili

Raul Jimenez aliipa Benfica bao la kwanza katika dakika ya 27. Hata hivyo, Arturo Vidal aliisawazishia Munich katika dakika ya 37, na Thomas Müller akaiweka kifua mbele katika dakika ya 52. Talisca alisawazisha katika dakika ya 76 lakini Munich ikafuzu katika juhudi zake za kushinda taji la sita la Champions League, wakati Benfica wakirejea Lisbon.

Nchini Uhispania, Atletico Madrid iliwabandua nje mabingwa watetezi Barcelona kwa kuwazaba magoli mawili kwa sifuri. Magoli yote yalifungwa na mshambuliaji Muitaliano Antoine Griezmann. Atletico walifuzu kwa jumla ya mabao matatu kwa mawili. Barca ilikuwa ilishinda mchuano wa kwanza uwanjani Camp Nou bao moja kwa sifuri.

Bayern Munich na Atletico Madrid zimejiunga na Real Madrid ya Uhispania na Manchester City ya England katika droo ya nusu fainali itakayoandaliwa kesho Ijumaa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Caro Robi

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com