BASTI ABDULLAH :Kiongozi wa Lal Masjid aruhusiwa kuongoza sala ya mazishi | Habari za Ulimwengu | DW | 12.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BASTI ABDULLAH :Kiongozi wa Lal Masjid aruhusiwa kuongoza sala ya mazishi

Kiongozi wa msikiti wa Lal, Abdul Aziz ameruhusiwa kuongoza sala ya mazishi ya kakake Abdul Rashid Ghazi aliyeuawa na jeshi la Pakistan.Takriban watu alfu 2 wanahudhuria mazishi ya kiongozi huyo aliye na msimamo mkali wa Taliban aliyeuawa wakati msikiti mwekundu uliposhambuliwa na jeshi la Pakistan.

Rais Pervez Musharraf anatarajiwa kuhutubia taifa hii leo kueleza umuhimu wa hatua iliyochukuliwa ya kuvamia Msikiti wa Lal na madrassa ya watoto wa kike iliyokuwa karibu vilevile kupambana na ugaidi.

''Tuliposhambulia msikiti na kuudhibiti sasa wanatoroka katika vikundi vidogo kuelekea maeneo ya milimani.Kwahiyo tumevunjilia mbali mizizi yote ya kundi hilo.''

Wakati huohuo naibu kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Ayman al Zawahri anatoa wito kwa waislamu nchini humo kuendelea na Jihad ili kupinga serikali.

Msikiti huo ulitekwa baada ya ghasia kuzuka mwanzoni mwa mwezi huu kati ya polisi na wanafunzi wa msikiti huo walio na msimamo mkali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com