Bashir aahidi kuliunga mkono taifa jipya la Sudan Kusini | Matukio ya Afrika | DW | 29.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Bashir aahidi kuliunga mkono taifa jipya la Sudan Kusini

Matamshi hayo yamepokelewa vizuri na katibu mkuu wa kundi la waasi wa zamani SPLM, Pagan Amum

default

Rais wa Sudan, Omar el Bashir (kulia) na rais wa serikali ya Sudan kusini, Salva Kiir Mayardit

Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir ameahidi kulisaidia eneo la Kusini kuwa taifa lililostawi na imara endapo kura ya maoni ya mwezi ujao itaamua ijitenge na kujisimamia yenyewe.Katika hotuba maalum ya televisheni aliyoitoa akiwa eneo la Gezira, Rais Bashir alisema atakuwa wa kwanza kuitambua nchi hiyo endapo matokeo yataashiria kujitenga.

Kauli hizo zimepokelewa vizuri na katibu mkuu wa kundi la waasi wa zamani SPLM,Pagan Amum.Wakazi wa Eneo la Kusini mwa Sudan wanajiandaa kupiga kura ya maoni mnamo tarehe 9 itakayoiamua hatma yake itakayoitimiza azma yake ya kutaka kujitenga.

Kiasi ya wapiga kura milioni 3.5 wamesajiliwa kushiriki katika kura hiyo ya maoni.Wakati huohuo katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Amyr Moussa anaikamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Sudan alikokutana na viongozi wa kuisni na kaskazini.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com