1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barca yazidi kutanua mwanya La Liga

14 Januari 2013

Barcelona yazidi kukata mbuga kuelekea ubingwa wa La Liga , nchini Uhispania, na huko Uingereza Manchester United na Manchester City bega kwa bega katika ushindi.

https://p.dw.com/p/17JeQ
MADRID, SPAIN - AUGUST 29: (Back row L-R) Pedro Rodriguez, Javier Mascherano, Sergio Busquets, Gerard Pique, Victor Valdes (Front row L-R) Lionel Messi, Alexis Sanchez, Adriano Correia, Andres Iniesta, Xavi Hernandez, Jordi Alba of FC Barcelona pose for a team picture prior to the Super Cup second leg match betwen Real Madrid and FC Barcelona at Estadio Santiago Bernabeu on August 29, 2012 in Madrid, Spain. (Photo by David Ramos/Getty Images)
Kikosi cha FC BarcelonaPicha: Getty Images

Viongozi wa ligi ya Uhispania Barcelona wamekamilisha sehemu ya kwanza ya ligi hiyo kwa kujikingia points 55 kati ya 57 ambazo zilikuwa zinawaniwa katika sehemu ya kwanza ya ligi hiyo ,wakati Lionel Messi amefunga goli moja na kushiriki kutengeneza mengine mawili katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Malaga jana Jumapili(13.01.2013).

Ushindi huo wa 18 katika michezo 19 kwa kikosi cha kocha Tito Vilanova umeirejesha timu hiyo katika kuongoza kwa points 11 dhidi ya timu inayofuatia Atletico Madrid, ambao hapo mapema iliipata ushindi wake wa 10 katika michezo 10 iliyocheza nyumbani msimu huu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Zaragoza.

Real Madrid ambayo inatengana na Barca kwa points 18, ilitoka sare ya bila kufungana na Osasuna siku ya Jumamosi.

Nchini Uingereza Manchester United iliendelea kupeta na kufungua mwanya wa points saba dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili Manchester City , ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao Liverpool.

epa03218037 Manchester City's Samir Nasri (C-L) and Manchester City's Mario Balotelli (C-R) celebrate winning the Premier League at Etihad Stadium Manchester, Britain, 13 May 2012. EPA/PETER POWELL DataCo terms and conditions apply. http//www.epa.eu/downloads/DataCo-TCs.pdf +++(c) dpa - Bildfunk+++
Manchester City ya UingerezaPicha: picture-alliance/dpa

Manchester City ikaipiku Arsenal London kwa mabao 2-0 ukiwa ni ushindi wao wa kwanza nyumbani kwa Arsenal tangu mwaka 1975.

Chelsea inashikilia nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City.

Juventus Turin , ikiwa points nane mbele ya wapinzani wake katika Seria A kabla ya wakati wa Chrismas, points hizo zimenyofolewa na Lazio Rome hadi points 3 hivi sasa baada ya Juve kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Parma.

SSC Napoli iko nafasi ya tatu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Parlemo.

Olympique Lyon imenyakua nafasi ya kwanza katika League ya Ufaransa kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Troyes. Lyon inaongoza kwa points mbili zaidi ya Paris St German ambao walimudu tu sare ya bila kufungana na Ajancio.

Huko Ureno Benfica na Porto walitoshana sare ya mabao 2-2 katika mchezo mkali wa mahasimu hao jana Jumapili. Benfica Lisbon inaongoza ligi hiyo ikiwa na points 36 kutokana na michezo 14 hadi sasa, points tatu zaidi ya Porto.

Tamasha la mataifa ya Afrika.

Fainali za kuwania kombe la mataifa ya Afrika zinaanza rasmi siku ya Jumamosi wiki hii huko nchini Afrika kusini na kauli mbiu ya fainali hizi za Orange AFCON mwaka 2013 ni , "The beat at Africa's feet" , kwa tafsiri ambayo si rasmi sana ni , "mirindimo katika miguu ya Afrika".

Selecção Futebol 03.JPG Titel: Fußball-Nationalmannschaft der Kapverden vor dem Spiel gegen Kamerun Ort: Praia, Cabo Verde Fotograf: Daniel Almeida Datum: 08.09.2012 Beschreibung: Das Team aus den Kapverden vor dem Qualifikations-Spiel zur Afrika-Meisterschaft gegen Kamerun. Die Kapverden gewannen das Spiel mit 2:0. Die Kapverden haben sich 2012 zum ersten Mal für eine Afrika-Fußball-Meisterschaft qualifiziert. Die Inselrepublik wird in Südafrika 2013 zum ersten Mal an einem Africa Cup of Nations teilnehmen.
Kikosi cha timu ya taifa ya Cape VerdePicha: DW/Daniel Almeida

Watayarishaji wa fainali hizi wanasema kuwa , fainali hizi za 29 za AFCON nchini Afrika kusini zitakuwa za kupendeza kabisa. Mwenyekiti wa kamati ya utayarishaji wa fainali hizi nchini Afrika kusini Mwelo Nonkonyana amesema kuwa hakuna litakalosababisha kushindwa kwa fainali hizi.

"Tunataka kulihakikishia shirikisho la soka barani Afrika CAF, serikali yetu ya Afrika kusini, Waafrika na Waafrika kusini kwa jumla kuwa tuko tayari kuendesha mashindano haya ambayo yatakuwa ya kukumbukwa. Tuko tayari kuwapokea wachezaji wote , washirika wetu wa kibiashara, mashabiki wa kandanda na familia nzima ya mchezo wa soka".

Hata hivyo tikiti 860,000 ambazo ziko kwa ajili ya michuano hiyo , ni tikiti 320,000 tu ambazo hadi sasa zimekwisha nunuliwa.

Lakini tikiti 65,000 kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi baina ya Bafana Bafana , Afrika kusini na Cape Verde zimekwisha uzwa. Watayarishaji wa mashindano hayo wanamatumaini kuwa mauzo ya tikiti yataongezeka katika siku hizi zilizobaki kabla ya ufunguzi rasmi.

26 Mrz 2011JOHANNESBURG, SOUTH AFRICA - MARCH 26: South Africa starting team poses during the 2012 Africa Cup of Nations Qualifier match between South Africa and Egypt at Coca Cola Park on March 26, 2011 in Joh... Erfahren Sie mehrVon: Gallo ImagesKollektion: Getty Images Sport
Kikosi cha Bafana BafanaPicha: gettyimages

Sherehe za ufunguzi zitafanyika katika uwanja wa taifa mjini Johannesburg , uwanja ambao una uwezo wa kuingiza mashabiki 94,700.

Wakati Afrika inasubiria kwa hamu ufunguzi wa mashindano hayo makubwa katika bara la Afrika , mashabiki wa bara hilo wanasubiri kumtawaza mfalme mpya wa kutia mabao katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika atakayechukua nafasi ya Didier Drogba, ambaye huenda hii ikawa ni fainali yake ya mwisho, na pia Samuel Eto'o ambaye hatakuwako nchini Afrika kusini kwa kuwa timu yake ya Cameroon imeshindwa kufuzu kucheza katika fainali hizo.

Nani anaweza kuwa mfalme mpya wa kutia mabao basi, au kuna ukame wa washambuliaji hatari katika bara la Afrika hivi sasa?

Wakati huo huo mameneja wanalalamika katika bara la Ulaya , wakati wachezaji muhimu katika timu zao wanasafiri kwenda Afrika kusini kwa mashindano ya fainali za kombe la Afrika.

Mara hii tatizo hilo limeongezeka kutokana na mabadiliko ya kuendesha fainali hizo kutoka kila baada ya miaka miwili inayogawanyika na kuwa katika miaka isiyogawanyika, ikiwa na maana kulikuwa na miezi 12 tu baina ya fainali za mwaka jana na mwaka huu. Kuna mataifa 27 ya ulaya yanayowakilishwa katika fainali hizo, ikiwa ni pamoja na Liechtenstein na Luxembourg, na klabu kutoka Brazil, China, Japan na Marekani.

Ligi ya Ufaransa kwa kawaida inachangia wachezaji wengi katika fainali hizo, mara hii ikiwa na wachezaji 50, 15 wakitokea katika ligi daraja la kwanza, ambao watakosa michezo muhimu ya vilabu vyao kwa muda wa wiki tatu.

Kuna wachezaji 15 kutoka ligi kuu ya Uingereza, 14 kutoka Ureno, na 10 kutoka La Liga nchini Uhispania na 6 kutoka Serie A nchini Italia.

Sahin arejea Dortmund

Na katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji, katika kile kinachofahamika kama dirisha dogo la uhamisho kwa wachezaji duniani, Nuru Sahin mchezaji wa kiungo wa timu ya taifa ya Uturuki amejea nyumbani katika Bundesliga , katika timu ya Borussia Dortmund alikoanzia baada ya miezi 18 kufuatia vipindi ambavyo havikuwa na mafanikio katika klabu ya Real Madrid na Liverpool ya Uingereza.

DORTMUND, GERMANY - JANUARY 11: New player Nuri Sahin poses with chairman Hans Joachim Watzke and manager Michael Zorc during a Borussia Dortmund press conference at Signal Iduna Park on January 11, 2013 in Dortmund, Germany. (Photo by Lars Baron/Bongarts/Getty Images)
Nuri Sahin akitambulishwa na viongozi wa DortmundPicha: Bongarts/Getty Images

Hannover 96 ya Ujerumani imefanikiwa kupata saini ya mchezaji wa kati wa ulinzi Franca kutoka Brazil akitokea timu ya Coritiba.

Olympique Marseille nayo imefikia makubaliano na Newcastle United ya Uingereza kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Loic Remy.

Nae mchezaji wa timu ya taifa ya Urusi Andrei Yeshchenko amejiunga na Anzhi Makhachkala kutoka kwa mahasimu wao Lokomotiv Moscow.

Azarenka ndio namba moja

Na katika tennis , Victoria Azarenka anaanza kutetea taji lake la mchezo wa tennis la Australian Open akiwa juu ya orodha ya wachezaji bora iliyotolewa leo na shirikisho la mchezo huo duniani WTA. Maria Sharapova wa Urusi yuko katika nafasi ya pili , na Serena Williams wa Marekani yuko katika nafasi ya tatu.

Novak Djokovic, of Serbia, gestures to the crowd after defeating Pablo Andujar, of Spain, 6-0, 6-7 (5), 6-2, in a match at the BNP Paribas Open tennis tournament Wednesday, March 14, 2012, in Indian Wells, Calif. (Foto:Darron Cummings/AP/dapd) Victoria Azarenka, of Belarus, celebrates her 1-6, 7-6 (7), 7-5 win over Dominika Cibulkova, of Slovakia, during the Sony Ericsson Open tennis tournament in Key Biscayne, Fla., Monday, March 26, 2012. (Foto:Alan Diaz/AP/dapd)
Novak Djokovic na Victoria AzarenkaPicha: dapd/DW

Kwa upande wa wanaume Novak Djokovic amethibitishwa leo(14.01.2013) kuwa anaongoza orodha ya wachezaji wanaume wakati akianza kwa ushindi katika mashindano ya Australian Open , dhidi ya Paul-Henri Mathieu wa Ufaransa. Roger Federer wa Uswisi yuko katika nafasi ya pili na Andy Murray kutoka Uingereza anashikilia nafasi ya tatu.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre /dpae /ape / afpe

Mhariri: Yusuf Saumu