1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la usalama laiwekea vikwazo vipya Iran

Josephat Nyiro Charo10 Juni 2010

Kama ilivyotarajiwa baraza la usalama la umoja wa mataifa limeweka vikwazo vipya dhidi ya ran. Vikwazo hivyo vimelengwa kuzuwia uwezo wa kifedha wa jeshi la kimapinduzi la nchi hiyo

https://p.dw.com/p/NmrO
Rais wa Iran, Mahmoud AhmadinejadPicha: AP

Kwa kura za nchi kumi na mbili , mbili zimepinga na moja haikupiga kura , baraza la usalama la umoja wa mataifa baada ya miezi kadha ya ushauriano limeweka vikwazo vipya dhidi ya Iran.

Umoja wa mataifa unataka kuweka mbinyo zaidi kwa nchi hiyo kusitisha mpango wake unaoleta mvutano wa kinuklia. Lebanon haikupiga kura na Brazil na Uturuki zimepiga kura kupinga azimio hilo. Nchi hizo katikati ya mwezi Mei zilifikia muafaka kuhusiana na mpango huo wa Iran wa kinuklia. Vikwazo huenda vikawaathiri zaidi raia wa Iran.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeimarisha vikwazo vyake kutokana na azimio hili. Lengo la vikwazo hivyo, ambavyo ni vipya , ni kuzuwia uwezo wa kifedha wa jeshi la kimapinduzi nchini humo, ambalo linaudhibiti mkubwa wa mashirika na makampuni na ni mhimili mkubwa wa utawala wa Iran.

Azimio hili linawalenga maafisa wa jeshi hilo ambao akaunti zao zitazuiwa pamoja na kupigwa marufuku kusafiri. Marufuku pia imewekwa dhidi ya biashara ya silaha kama makombora, meli za kivita ama vifaru, na meli zinazoelekea nchini Iran zinaweza kufanyika ukaguzi, biashara zilizoko nje ya nchi hiyo zitawekewa mipaka. Iwapo benki moja ya Iran iliyoko nje ya nchi hiyo itatiliwa shaka , kuwa inamahusiano na mpango wa kinuklia, pia itakumbwa na vikwazo hivyo.

Marekani, Uingereza , Ufaransa na Ujerumani zimelenga kwa maksudi sekta hii ya nishati katika hatua zilizochukuliwa za adhabu. Urusi yenye kura ya turufu pamoja na China hata hivyo baada ya hapo hazikuungana na mataifa hayo. Hata hivyo balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice amesema azimio hilo lilikuwa ni mihumu na sahihi.

Susan Rice
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan RicePicha: picture alliance / landov

Kwa sababu serikali ya Iran imechagua kwa uwazi na bila kulazimishwa, kuendea kinyume wajibu wake katika shirika la IAEA, na maazimio ya baraza hili.

Balozi wa Ujerumani katika umoja wa mataifa Peter Wittig, ameiweka hali kuwa moto zaidi kwa kusema kwamba azimio hilo kwa upande wa Iran ni nafasi nyingine mpya pia ya kuendelea na mazungumzo.

Tunamatumaini , kuwa Iran sasa itapokea mkono huu ulionyooshwa kwake na kuanza mazungumzo juu ya mpango wake wa kinuklia.

Hata rais Barack Obama wa Marekani anathibitisha hayo, kwa kusema, mlango uko wazi kwa mazungumzo ya kidiplomasia kutokana na vikwazo hivi vipya. "Tunafahamu kuwa serikali ya Iran haitabadili tabia yake kwa siku moja. Lakini kura iliyopigwa leo, inaonyesha msimamo unaozidi kuongezeka ambao utasababisha Iran kulipia ukaidi wake."

Hii ni duru ya nne sasa ya vikwazo dhidi ya Iran kuanzia Desemba 2006. umoja wa mataifa , unahofia kwamba , nchi hiyo kwa kujificha katika pazia la mradi wa utafiti wa nishati kwa matumizi ya kiraia inataka kujenga uwezo wa kuunda silaha za atomiki. Hadi sasa nchi hiyo haijasitisha urutubishaji wake wa madini ya uranium na madai ya shirika la umoja wa mataifa la nishati ya atomic hayajafanikiwa.

Iran inaonyesha kuwa hadi sasa haijafikiwa na mbinyo wa kimataifa. Hatujali maazimio mangapi yatapitishwa, tutaendelea na urutubishaji wa madini ya uranium, amesema mwanadiplomasia mmoja wa Iran baada ya kura katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Mwandishi : Bodewein, Lena / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo