1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama la UN laiongezea muda MONUSCO huko DRC

20 Desemba 2025

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kuongeza muda wa kuhudumu kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO).

https://p.dw.com/p/55kac
Goma | Askari wa MONUSCO wakiwa katika msafara mashariki mwa DRC
Askari wa kulinda amani wa MONUSCO wakiwa katika msafara huko Goma, mashariki mwa DRCPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Azimio hilo lilipigiwa kura Ijumaa na kikosi hicho kimeongezewa muda wa mwaka mmoja wa ziada hadi Disemba 20, 2026 huku Marekani ikitoa wito kwa vikosi vya Rwanda na waasi M23 kuheshimu makubaliano ya amani ya kikanda kufuatia vurugu zinazoendelea kushuhudiwa mashariki mwa DRC.

Mwakilishi wa Marekani katika mkutano huo Jennifer Locetta, amesema "mazungumzo ya kuiongezea muda MONUSCO yalitiwa kiwingu na mwenendo wa Rwanda na waasi wa M23 wa kuhujumu mchakato thabiti wa amani."

Kikosi cha  MONUSCO  chenye wanajeshi 11,500 ni moja ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vinavyoungwa mkono na Marekani. Lakini utawala wa rais Donald Trump ulijaribu kupunguza mchango wake wa kifedha kwa Umoja wa Mataifa hasa katika eneo la ulinzi wa amani duniani.