1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la usalama kuidhinisha duru ya tatu ya vikwazo dhidi ya Iran

3 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DGl0

NEW-YORK

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa leo hii linatazamiwa kuidhinisha duru ya tatu ya vikwazo dhidi ya Iran kufuatia nchi hiyo kukataa kusimamisha shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe katika baraza hilo wanasema hakuna uhakika ikiwa vikwazo hivyo vipya vitaungwa mkono na wengi kama ilivyofanyika katika maazimio mawili ya mwanzo yaliyopitishwa baraza hilo.

Nchi tano za wanachama wa kudumu katika baraza hilo zenye kura ya turufu,Marekani,China,Uingereza,Urussi,na Ufaransa zinaunga mkono azimio hilo jipya na zinaidadi ya zaidi ya kura tisa za ndio ambazo zinahitajika kuidhinisha vikwazo hivyo katika baraza hilo lenye wanachama 15.Hata hivyo wanachama wengine ambao sio wakudumu kwenye baraza hilo kama Libya,Indonesia;Afrika Kusini na Vietnam zimezungumzia wasiwasi wake juu ya hatua hiyo.Jumamosi iliyopita Ufaransa na Uingereza zilikhairisha shughuli ya kupigia kura azimio hilo ili kuzishawishi nchi hizo zenye wasiwasi kukubali hatua hiyo lakini baadhi ya wajumbe wanasema haitowezekana.