Baraza la Mawaziri Niger lajiuzulu. | Matukio ya Kisiasa | DW | 01.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Baraza la Mawaziri Niger lajiuzulu.

Serekali ya Rais Mamadou Tandja wa Niger imevunjwa kutokana na kukosa imani ya wabunge wa nchi hio.

Ramani ya Niger

Ramani ya Niger

Waziri Mkuu wa Niger Hama Amadou, ambae amekua madarakani miaka saba ,itambidi sasa angatuke madarakani kwa sababu, kiini cha mzozo wote kimeanzia kwake .

Niger ni nchi yenye utajiri mwingi, wa madini

ya Urenium lakini nchi hio, ni moja ya nchi zilizokua masikini Duniani.

Jana bunge la Niger lilipiga kura yakutokua na imani na Serekali ya waziri mkuu, Hama Amadou, baada ya wapinzani kuilaumu Serekali hio, kwa visa vya rushwa na ubadhirifu wa Fedha za umma .

Bunge la Niger lina wabunge 113 na 62 kati ya hao, walipiga kura ya kutokua na imani na Serekali ya waziri mkuu wa Niger.

Kutokana na katiba ya nchi hio, moja kwa moja, waziri mkuu na baraza lake wote , inabidi wajiuzulu. Na waziri mkuu leo anatarajiwa kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais wa Niger Mamadou Tandja.

Wapinzani wa waziri mkuu wamekua

wakimlaumu, Hama Amadou, kuuiba Dollar millioni Moja na laki mbili, pesa zilizotolewa na wafadhili, kusaidia ukarabati wa Shule za nchi hio.

Kashfa hii imewahusu pia mawaziri wawili waliokua wa wizara ya Elimu, ambao mwaka jana walitiwa mbaroni lakini mpaka sasa bado hawajafikishwa mahakamani; lakini Bw Amadou amekua akiyakanusha madai hayo ya wapinzani kuhusu rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma, na kwamba amefanya njama za chini kwa chini ili mawaziri hao wawili, wasifikishwe mahakamani.

Rais Mamadou Tandja wa Niger sasa anakabiliwa na jukumu la kumteua waziri mkuu mpya au kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mkuu kwa siku Arubaini na tano kuanzia sasa.

Mohd Bazoum ambae ni makamu rais wa chama kiku cha upinzani cha Niger Democracy and Socialism akiwa pamoja na wapinzani wengine, wamesema hawatochukua uamuzi wa kumchagua mtuu kutoka upande wao ili ateuliwe kua waziri mkuu, lakini madaraka yote wanamuachia Rais Mamadou Tandja ateue mgombea kutoka chama chake cha National Movement for Development of

Society (MNSD)

Nchi ya Niger ina idadi ya watu millioni tatu na laki sita, na nchi hio imekua ikikabiliwa na ukame wa kila mara na kulifanya taifa hilo kua miongoni mwa mataifa maskini Duniani., na hali Niger ndio nchi ya tatu duniani kua na utajiri wa maadini ya Urenium.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com