1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGUI : Waasi na serikali wasaini makubaliano ya amani

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVM

Kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati hapo jana amewataka wapiganaji wake kuweka chini silaha zao baada ya kusaini makubaliano ya amani na Rais Francois Bozize.

Abdoulaye Miskine kiongozi wa chama cha Peoples’ Demokratik Front ambacho ni mojawapo ya kundi la waasi lililosaini makubaliano hayo na Bozize nchini Libya hapo Ijumaa ameliambia shirikia la habari la Uingereza Reuters kwamba wale watakaopuuza amri yake wataadhibiwa.

Katika mahojiano mjini Bangui baada ya kuwasili kutoka Libya Miskine ametowa wito kwa wapiganaji wake walioko vichakani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,Sudan,Chad na Cameroon kusalimisha silha zao na kuungana naye na kwamba wale watakaokaidi amri yake watakiona cha moto.

Makubaliano hayo ya amani yanawataka waasi waache operesheni za kijeshi na serikali badala yake imekubali kuwapa msamaha waasi hao na kuruhusu kujumuishwa kwa wanajeshi wake katika jeshi la taifa.