1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bangui. Serikali yatia saini makubaliano na waasi.

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCA3

Serikali ya jamhuri ya Afrika ya kati imetia saini makubaliano ya amani na waasi wa Union of Democratic Forces Coalition.

Jenerali Raymond Ndoungou amekwenda katika ngome ya kundi hilo la waasi katika mji wa Birao ili kutia saini makubaliano hayo kwa niaba ya serikali.

Damane Zakaria , mkuu wa kijeshi wa kundi la UFDR alitia saini kwa niaba ya waasi.

Chini ya makubaliano hayo, kundi la waasi la UFDR litaingizwa katika jeshi la taifa. Kwa kufanya hivyo , serikali imekubali kundi la UFDR kuwa chama cha kisiasa, ambacho kitachangia katika utawala wa nchi hiyo kwa masharti kuwa kinaacha mapambano ya silaha.