BANGKOK: Watu wawili wauwawa katika mashambulio ya mabomu | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BANGKOK: Watu wawili wauwawa katika mashambulio ya mabomu

Watu wawili wameuwa leo mchana kufuatia milipuko sita ya mabomu mjini Bangkok nchini Thailand. Duru za polisi zimearifu kwamba watu wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo. Kufikia sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mashambulio hayo.

Mabomu yote sita yamelipuka katika muda wa saa moja, mlipuko mbaya ukiwa ule uliotokea baada ya bomu lililotegwa chini ya kiti kwenye kituo cha basi nje ya duka kubwa, kulipuka na kuwajeruhi watu 15, wawili kati yao vibaya.

Bomu lengine liliripuka nje ya kituo cha polisi na kuwajeruhi watu wawili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com