1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGKOK : Wakubaliana kupiga vita mabadilko ya hali hewa

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC52

Wataalamu wa mabadiliko ya hali ya hewa wanaokutana katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini Bangkok Thailand wamefikia makubaliano mapema leo hii juu ya njia bora za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Repoti hiyo ya Jopo la Kiserikali la Kimataifa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa ambayo lazima iidhinishwe kwanza imekuja baada ya mjadala wa muda mrefu wa faragha.Rasimu ya mwisho bado haikuweza kupatikana lakini wajumbe wanasema kwamba kwa kiasi kikubwa inafanana na rasimu iliokuwa ikiitaka dunia kuachana na matumizi ya nishati nzito za carbon dio oxide kama vile makaa na badala yake kutumia nishati za teknolojia za ufanisi pamoja na kupunguza ukataji misitu kwa kiasi kikubwa.

Tokea Jumatatu wanasayansi na wataalamu kutoka nchi 120 wamekuwa wakijadili namna ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa katika mji mkuu wa Thailand Bangkok.