BANGKOK: Miripuko ya mabomu yasababisha maafa nchini Thailand | Habari za Ulimwengu | DW | 01.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BANGKOK: Miripuko ya mabomu yasababisha maafa nchini Thailand

Watu watatu wameuawa na wengine takriban thelathini wakajeruhiwa wakiwemo raia sita wa kigeni baada ya wimbi la mashambulio ya mabomu katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok.

Mabomu sita yaliripuka jana katika maeneo kadha ya mji huo na kusababisha serikali kufutilia mbali mipango ya kusherehekea mwaka mpya.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na miripuko hiyo lakini polisi wanaamini huenda wahusika ni wanamgambo wanaotaka kujitenga kusini mwa nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com