Ban Ki Moon aeleza wasiwasi wake kuhusu Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 26.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ban Ki Moon aeleza wasiwasi wake kuhusu Kosovo

LJUBLJANA: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameeleza wasiwasi wake kuhusu mfarakano uliozuka katika Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu mustakabali wa jimbo la Kosovo.Baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Slovenia Janez Jansa ambae hivi sasa pia ni Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya,Katibu Mkuu Ban alisema,kuna hatari ya Kosovo kujiamulia yenyewe mustakabali wake,iwapo mvutano huo utaendelea katika Baraza la Usalama.

Jimbo la Serbia la Kosovo lililo na wakaazi wengi wenye asili ya Kialbania limeshasema kuwa litajitangazia uhuru wake hivi karibuni.Jimbo hilo lipo chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1999.Marekani na baadhi kubwa ya nchi za Umoja wa Ulaya zinaunga mkono uhuru wa Kosovo.Lakini Serbia na Urusi iliyo na kura ya turufu,zinaendelea kupinga uhuru wa jimbo la Kosovo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com