1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban aonya kushindwa shughuli za amani Dafur

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYhq

NEW YORK

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon ameonya kwamba shughuli za kulinda amani huko Dafur nchini Sudan zinaweza kushindwa venginevyo msaada wa kutosha unatolewa kwa kikosi cha kulinda amani cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Akizungumza mjini New York Ban amesema shughuli hizo zinaweza kukwama kabla ya hata kuanza.

Shughuli hizo za Umoja wa Mataifa ambazo zitaendeshwa kwa pamoja na Umoja wa Afrika zilikuwa zinatazamiwa kuanza huko Dafur katika kipindi cha wiki tatu zijazo ambapo kikosi kikubwa zaidi cha wanajeshi 20,000 kikitazamiwa kuwekwa hapo mwezi wa Januari mwakani.

Takriban watu 300,000 wameuwawa tokea mwaka 2003 kutokana na mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na waasi.

Watu huanza kufikiria kuwa hicho ni kitu cha kawaida katika maisha kwamba inabidi moja kwa moja wagharimike sana katika maisha na kwa hiyo wanakuwa hawawezi kukataa.