1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban afadhaishwa na Darfur

6 Septemba 2007

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema hapo jana amefadhaishwa na kujisikia dhalili kutokana na ziara yake kwenye kambi ya wakimbizi huko Dafur ambapo maelfu walimshangilia wakati alipoahidi kuimarisha juhudi za kuleta amani kwenye jimbo hilo la Sudan lililoathiriwa na vita.

https://p.dw.com/p/CB1U
Ban Ki Moon akiongea na wafanyakazi wa UN
Ban Ki Moon akiongea na wafanyakazi wa UNPicha: AP

Ban yuko nchini Sudan kuupa nguvu mchakato wa amani ya Dafur na amewaambia waandishi wa habari kwamba ameweza kupiga hatua ya maendeleo katika kupanga tarehe na mahala pa kufanyika mazungumzo hayo ya amani kati ya serikali ya Sudan na takriban makundi 12 ya waasi wa Dafur.Ban amesema Umoja wa Mataifa lazima ulinde haki za binaadamu na kwamba kila hatua ichukuliwe kuhakikisha kwamba wakimbizi milioni mbili huko Dafur wanaweza kurudi nyumbani kwao na katika ardhi yao.

Kikosi mchanganyiko cha kulinda amani cha wanajeshi 26,000 wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kinatazamiwa kuandamana na mchakato huo wa amani.