BAMAKO: Rais wa Guinea amemteua waziri mkuu mpya | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAMAKO: Rais wa Guinea amemteua waziri mkuu mpya

Rais Lansana Conte wa Guinea anaekabiliwa na upinzani nchini,amekubali kumteua waziri mkuu mpya atakaekuwa na usemi mkubwa.Makubaliano hayo kati ya rais Conte na viongozi wa vyama vya wafanyakazi huenda yakasaidia kumaliza mgomo mkuu wa majuma mawili uliosababisha vifo vya si chini ya watu 60.Nchi hiyo ya Afrika Magharibi haina waziri mkuu tangu mwezi wa Aprili mwaka jana, baada ya rais Conte kumfukuza kazi kiongozi wa serikali.Wananchi wa Guinea kwa maelfu na elfu baada ya kuanza kuandamana tarehe 10 mwezi wa Januari kulalamika dhidi ya matatizo magumu ya kiuchumi,viongozi wa vyama vya wafanyakazi walitoa mwito wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya. Waandamanaji wengi vile vile wametoa mwito wa kumtaka rais Conte ajiuzulu.Conte anatawala nchini Guinea tangu mwaka 1984.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com