1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Balozi wa Rwanda aikosoa Uingereza juu ya haki za binadamu

Zainab Aziz
2 Oktoba 2023

Balozi wa Rwanda nchini Uingereza amerekodiwa jijini London kwa siri akiikosoa Uingereza na historia yake ya haki za binadamu. Amesema waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza hayuko sahihi kabisa kuhusu swala la uhamiaji.

https://p.dw.com/p/4X2u5
Großbritannien Gerichtsurteil gegen Pläne der Regierung zur Abschiebung nach Ruanda
Picha: Tom Pilgrim/empics/picture alliance

Balozi wa Rwanda nchini Uingereza Johnston Busingye, ambaye zamani alikuwa waziri wa sheria wa Rwanda, alirekodiwa kwa siri na kikundi cha kampeni cha LBD, "Led By Donkey” ambapo aliilaumu Uingereza kwa matendo yake ya ukiukaji wa haki za binadamu kwa karne nyingi huku akipuuzia kuhusu mwenendo wa kisiasa wa nchi yake.

Uingereza imeidhinisha mpango wa ushirikiano kati yake na Rwanda kuhusu wahamiaji ambapo Uingereza itawapeleka nchini Rwanda maelfu ya wahamiaji wanaowasili mara kwa mara katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo kwa boti ndogo ndogo kutoka kaskazini mwa Ufaransa.

Raia wa Uingereza akipinga nchi yake kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda
Raia wa Uingereza akipinga nchi yake kuwapeleka wahamiaji nchini RwandaPicha: Niklas Hallen/AFP

Hata hivyo, mpango huo unakosolewa vikali na makundi ya kutetea haki za binadamu na wadau wengine na hadi kufikia sasa umekwama kutokana na kukabiliwa na pingamizi kwenye mahakama nchini Uingereza.

Soma pia: Mpango wa serikali ya Uingereza wa kurahisisha kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda, unatazamiwa kuwa sheria

Wakati huo huo, waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Suella Braverman mara kadhaa amezua utata kuhusu swala la uhamiajnakwa mfano hivi majuzi alihoji iwapo Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi unafaa kuendelea kutumika katika zama hizi.

Uingereza, na Waziri wake wa mambo ya ndani Suella Braverman wanasisitiza kuwa Rwanda ni nchi salama zaidi ulimwenguni ya kuwapeleka watu wanaotafuta hifadhi na wakimbizi, licha ya ushahidi wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.

Katika mkanda wa video uliorekodiwa kwa siri, balozi Busingye alionekana kupuuzilia mbali wasiwasi juu ya mauaji ya wakimbizi hapo awali nchini Rwanda.

Kushoto: Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman. Kulia: Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Kushoto: Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman. Kulia: Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi SunakPicha: Frank Augstein/empics/picture alliance

Alipoulizwa ni kipi ambacho angemwambia Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Waziri wa mambo ya ndani Suella Braverman juu ya msimamo yao kuhusu wahamiaji.

Balozi wa Rwanda nchini Uingereza Johnston Busingye alisema angewaambia moja kwa moja kuwa "wanakosea kabisa" na kwamba wanachopaswa ni kuwa na sera ya muda mrefu ya kuwafanya watu waslifanye kuwa ni chaguo lao kusafiri na kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya kuja Uingereza.

Soma pia: Waziri Mkuu wa Uingerezaa apata pigo baada ya mahakama kubatilisha mpango wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda imesema ni kinyume cha sheria.

Balozi huyo aliongeza kusema kwamba wahamiaji wanakuja ulaya kwa sababu hawana matumaini. Amerekodiwa akisema ni kinyume cha maadili kwa Uingereza kuendelea kujiona kama nchi ya wakimbizi, nchi ya faraja, nchi ya ulinzi na ya huruma.

Amekumbusha kwamba waingereza waliwatumbukiza kwenye utumwa mamilioni ya watu kwa miaka 400. Amesema Waliziharibu India, China na hata bara la Afrika kutokana na historia ya kifalme ya Uingereza.

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul KagamePicha: Estácio Valoi/DW

Serikali ya Rwanda imejibu taarifa hiyo ya kundi la Led By Donkey, kwa kusema yapo makosa kadhaa kwenye taarifa hiyo iliyorekodiwa kwa siri ya dakika 24 na kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii. Imesema Rwanda ni mahala pazuri pa kuwaunga mkono wale wanaotafuta usalama na furs ana kwamba nchi hiyo imejitolea kwa kuzingatia kanuni ya kumpa kila mtu haki sawa.

Chanzo: AFP